Ongeza uwezo wako wa kufanya biashara kwa spreads ndogo zaidi za indices za Marekani za Exness
Na Paul Reid
19 Desemba 2024
Kila trader mwenye uzoefu angependa spreads ndogo na ni dhamira ya taasisi zote za kifedha kupata usawa unaofaidi traders na wawekezaji. Spreads, kama bei za duka, zinaweza kutofautiana kutoka kampuni moja hadi nyingine, lakini umuhimu wake haupaswi kupuuzwa. Kadiri spread ilivyo chini, ndivyo gharama ya biashara inavyopungua… na gharama za biashara zinapopungua, hasara hupungua na faida zinazowa kupatikana huongezeka. Ni uhusiano rahisi wa sababu na athari ambao traders wa kitaalamu wanafahamu sana.
Tunajua ni nini muhimu kwa traders kwa sababu tunawasikiliza. Exness ilipoanza mwaka wa 2008, waanzilishi walikuwa na maono moja kuu. Kuendesha maendeleo ya kiteknolojia, kuwa wabunifu na kutoa masharti bora za biashara, zana na vipengele kuliko broker mwingine yeyote duniani. Imepita miaka 17 na tumekua sana, lakini bado tumejitolea kuwapa traders wetu uzoefu bora zaidi wa biashara, ambao unatuleta kwenye sasisho la hivi punde kuhusu spreads kwa Indices za Marekani.
Tunajivunia kutangaza kuwa tumefanya trade ya indices za Marekani kuwa bora zaidi kwako kwa kupunguza spreads kwenye indices kuu, ikiwa ni pamoja na Dow Jones Industrial Average (US30), S&P 500 (US500), au NASDAQ-100 (USTEC).
Kufikia sasa, utaokoa 67% kwenye spreads zako unapofanya trade kwenye indices hizi kuu—hilo ni punguzo kubwa ambalo hunufaisha moja kwa moja utendaji na mfuko wako, kwa kupunguza gharama zako na kuboresha uwiano wa faida.
Bila shaka, spreads zinaweza kubadilika na kupanuka kutokana na sababu zikiwemo volatility na liquidity ya soko, matoleo ya habari, matukio ya kiuchumi, wakati masoko yanafunguliwa au kufungwa na aina ya instruments zinazofanyiwa trade, lakini misingi inashushwa ili kukupa uwiano na uzoefu bora wa biashara.
Hatujaribu tu kufikia viwango vya tasnia—tunaviweka. Wakati wowote unapofanya trade kwenye indices kuu katika Exness, unafanya trade kwa masharti ya kipekee yanayolengwa kukufaidi.
Tunaelewa changamoto ambazo traders wote wanakabiliana nazo na kipaumbele chetu ni kukupa zana na masharti ya biashara ambayo yatakusaidia kushinda changamoto hizo. Unapofanya trade katika Exness, unachagua broker ambaye amejitolea sana kwa mafanikio yako na hii inaweza kuonekana katika spreads zetu za kipekee. Katika Exness, haufanyi trade tu—unakua na kujenga mustakabali wenye fursa nyingi sana.
*Kupunguzwa kwa spreads kunarejelea spreads katika akaunti za Pro, kuanzia tarehe 5 Oktoba 2024 na kuendelea.
Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio ubashiri wa matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya trade kwa kuwajibika.
Mwandishi:
Paul Reid
Paul Reid ni mwandishi wa habari za kifedha aliyejitolea kufichua miunganisho ya kimsingi iliyofichwa ambayo inaweza kuwapa traders faida. Akilenga zaidi soko la hisa, hisia za Paul za kutambua mabadiliko makubwa ya kampuni zimethibitishwa vyema kutokana na kufuata masoko ya kifedha kwa zaidi ya muongo mmoja.