Maarifa

Je, ni mwisho wa utafutaji wa Google?

Na Paul Reid

16 Mei 2024

google search end

Huhitaji orodha ndefu ya indicators ili kuona trend ya sasa ya GOOGL. Fungua akaunti ya demo ya Exness kwenye Eneo lako la Binafsi la Exness na tufanye ubashiri.

Ya kwanza ni Moving Averages. Zana ya Moving Averages huonyesha ishara dhabiti ya ununuzi katika vipindi mbalimbali. Simple na Exponential Moving Averages (SMA na EMA) kwa vipindi 5, 10, 20, 50, 100 na hata 200 vinaonyesha ishara ya ununuzi. Hii ni indicator ya wazi ya mwenendo dhabiti wa kupanda kwa bei ya stock.

Indicators za Kiufundi

Indicators zingine kadhaa za kiufundi pia zinaunga mkono ishara hii ya ununuzi.

 • Relative Strength Index (RSI): 66.35, ikionyesha kuwa stock hiyo bado haijanunuliwa kupita kiasi.
 • MACD (12,26): 0.84, inapendekeza mwenendo wa kupanda.
Volatility
 • Average True Range (ATR) iko karibu 0.90, kuonyesha volatility ya chini, ambayo inaweza kuwa nzuri kwa mienendo thabiti ya bei.
Points za Mabadiliko

Kutumia points za mabadiliko kunaweza kusaidia kutambua support na resistance levels.

 • Support Level: S1: $170.51
 • Resistance Level: R1: $172.65

Indicators za kutumia wakati wa kubashiri GOOGL

Moving Averages
 • Ongeza Simple Moving Averages (SMA) kwa vipindi 10, 20, 50, 100 na 200.
 • Ongeza Exponential Moving Averages (EMA) kwa vipindi 10, 20, 50, 100 na 200.

Hizi zitakusaidia kufuatilia trends za bei ya stock katika timeframes tofauti.

Relative Strength Index (RSI)
 • Weka RSI kwa vipindi 14 ili kupima mwenendo wa stock na kutambua hali ya kununuliwa au kuuzwa kupita kiasi.
Moving Average Convergence Divergence (MACD)
 • Tumia mipangilio ya kawaida (12, 26, 9) ili kutambua mwenendo wa kupanda au kushuka.
Ultimate Oscillator
 • Weka kwa kutumia vigezo (7, 14, 28) ili kupima mwenendo wa bei katika timeframes tofauti.
Mifumo ya vinara
 • Tafuta mifumo ya kawaida kama vile mfumo wa Engulfing wa Kupanda kwa Bei, mfumo wa Hammer wa Kupanda kwa Bei na mfumo wa Doji. Mifumo hii inaweza kuashiria mabadiliko au miendelezo yanayoweza kutokea.
Points za Mabadiliko
 • Ongeza points za mabadiliko ili kubaini support na resistance levels. Tumia ukokotoaji wa point ya kawaida ya mabadiliko.
Bollinger Bands
 • Zitumie ili kuibua volatility na kutambua points zinazowezekana za breakout.
Fibonacci Retracement:
 • Ongeza zana hii kwenye chati ili kubaini support and resistance levels zinazoweza kutokea kulingana na mabadiliko ya kihistoria ya bei.

Kwa kuunganisha baadhi ya indicators na zana hizi, utaunda chati ya uchanganuzi wa kiufundi iliyokamilika vizuri ambayo inatoa maarifa kuhusu trends za bei, mwenendo, volatility na points za mabadiliko zinazoweza kutokea.

Google katika siku zijazo

Siku zijazo za Google, haswa utendaji wake wa msingi wa utafutaji, zimeunganishwa na mabadiliko ya AI. Ingawa AI ya uzalishaji inabadilisha utafutaji, Google bado imejitolea kudumisha matokeo ya utafutaji ya kiwango cha juu kwa kutoa vyanzo mbalimbali na kushughulikia wasiwasi kuhusu maudhui yanayotokana na AI.

Uzinduzi wa hivi majuzi wa zana za AI kama vile ChatGPT umeifanya Google kujitetea, na hivyo kuzua maswali kuhusu uwezo wake wa kuvumbua na kuzoea. Hata hivyo, mbinu ya utaratibu na maono ya Pichai inalenga kuimarisha uwezo wa AI kudumisha na kuimarisha nafasi ya Google.

AI inapoendelea kubadilisha tasnia ya kiteknolojia, mkakati wa Google chini ya uongozi wa Pichai unazingatia uvumbuzi, kuzoea, na maono wazi ya siku zijazo. Ujumuishaji wa AI katika operesheni zote za Google unaashiria dhamira ya kampuni ya kuongoza awamu inayofuata ya maendeleo ya kiteknolojia. Hata hivyo, kasi ya juu ya ukuaji wa AI na ushindani kutoka kwa wapinzani kama Microsoft zinaonyesha hitaji la mabadiliko endelevu ya mikakati ya kudumisha uongozi wake katika soko.

Google inapozindua vipengele vipya vya AI na kukabiliana na shinikizo za ushindani, traders na wawekezaji hufuatilia kwa karibu mabadiliko haya. Kuanzishwa kwa zana za AI na washindani kumeathiri hisia za soko, na kusababisha kubadilika kwa bei ya stock ya GOOGL. Maendeleo yanayoendelea na majibu ya kimkakati ya Google yatachukua jukumu kubwa katika kubainisha utendaji wa stock zake na nafasi ya soko katika siku zijazo zinazotawaliwa na AI.

Hitimisho

Uvumi unaweza kuathiri hisia za soko, lakini ikiwa chanzo cha kushuka kwa bei hakina athari za muda mrefu, kampuni kubwa huonekana kurejea baada ya muda mfupi baada ya mambo kutulia. Dhana kwamba vyanzo vikuu vya pesa vya Google (utafutaji na matangazo ya YouTube) vitafilisika kwa sababu ya AI ni potofu.

Ingawa Bard/Gemini zilikuwa na mwanzo mbaya, utendaji unabadilika na kuna uwezekano wa kuwa sehemu kubwa ya maisha yetu katika miezi na miaka ijayo. Isipokuwa ikiwa Wavuti ya Ulimwengu Wote utaanguka kabisa, Google ina nafasi kubwa katika siku zetu zijazo na bei za stock zitaonyesha hilo. Kumbuka tu kwamba hisia za soko zitaathiriwa na changamoto ndogo, kwa hivyo usitarajie mwenendo usiobadilika wa kupanda.


Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio ubashiri wa matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya trade kwa kuwajibika.


Mwandishi:

Paul Reid
Paul Reid

Paul Reid ni mwandishi wa habari za kifedha aliyejitolea kufichua miunganisho ya kimsingi iliyofichwa ambayo inaweza kuwapa traders faida. Akilenga zaidi soko la hisa, hisia za Paul za kutambua mabadiliko makubwa ya kampuni zimethibitishwa vyema kutokana na kufuata masoko ya kifedha kwa zaidi ya muongo mmoja.