Elimu

Mafanikio katika biashara: je, kuna fomula isiyo ya kawaida?

Na Paul Reid

12 Januari 2024

2705 trading success formula

Umewahi kushangaa kama biashara inakufaa? Labda swali halisi ni: je, unafaa kwa biashara? Je, kuna fomula isiyo ya kawaida inayofanya trader mmoja kufanikiwa wakati wengine wanahangaika? 

Baadhi ya watu wanaamini kuwa mtazamo au tabia maalum hutenganisha traders wa kiwango cha juu na wengine. Wengine wanasisitiza kuwa kinachohitajika ni kupata elimu inayofaa. Kisha kuna wale wanaosema kuwa "pesa hutengeneza pesa" na kuwa huwezi kupata pesa ikiwa huna nyingi za kuanzia kutrade nazo. Na tusisahau bahati ya kawaida na rahisi: sharti uwe mahali panapofaa kwa wakati unaofaa, kweli?  Kwa kuzingatia hayo yote, nina hadithi, na asili yake ni Omaha, Nebraska, nchini Marekani.

Mvulana alizaliwa katika ulimwengu ulioathirika pakubwa kutokana na Great Depression. Huku akiwa na mwerevu na udadisi wa kiwango cha juu, mvulana huyu alianza safari yake si kwa utajiri bali kwa nia ya kushinda nambari fulani ambazo zilionekana kudhibiti watu wazima pakubwa. Nambari ambazo ziliamua ni nani atakayefanya kazi hadi kufa na nani atakayeishi maisha bora.

Katika umri mdogo wa miaka sita, huku watoto wengine wakicheza na askari wa midoli na marumaru, alikuwa akiandika nambari kwenye mabango ya duka la mboga la babu yake, tayari akikokotoa margins za faida na gharama.

Kila mtu alijua kuwa mvulana huyo alikuwa tofauti na wengine. Shughuli yake ya burudani aliyoipenda sana ilikuwa biashara, kuuza peremende na soda, huku akifurahia kila faida aliyopata. Akiwa na umri wa miaka 11, huku watoto wengine wa umri wake wakifurahia kusoma vitabu vya katuni, alijaribu kwa mara yake ya kwanza kuwekeza kwenye soko la hisa, na kuwekeza katika hisa tatu za stock zake mwenyewe alizopendelea za Cities Service na tatu kwa niaba ya dada yake. Mwelekeo wa maisha yake tayari ulikuwa wazi, lakini safari yake haikuwa rahisi. 

Akiwa kijana, alikuwa amehisi uchungu wa kukataliwa na Shule ya Biashara ya Harvard. Lakini katika kumbi za Columbia, wawekezaji wawili waliobobea, Benjamin Graham na David Dodd, walibadilisha kila kitu. Walimpa umakini na madhumuni yaliyopangwa, na maarifa yake yalikua hadi uelewa wake kile kinachoongoza soko ukawa wa kiwango cha juu zaidi.

Katika miaka iliyofuata, alikabiliana na hatari kutokana na volatility ya soko na mwaka baada ya mwaka, aliibuka mshindi huku wengine waliokuwa karibu naye wakiyumba. Kisha akapata lengo kubwa kuliko kufanya trade ya masoko pekee, na akaanza ushirikiano wake wa kwanza. Ofisi yake ilikuwa chumba chake cha kulala na washirika wake walikuwa familia yake - mwanzo wa kiwango cha chini.

Miaka ilipita na akabobea zaidi katika uwekezaji. Angeweza kuhisi mtiririko wa uchumi, kufuata mawimbi ya trends, na kuchukua hatua kabla ya mabadiliko kutokea. Ushirikiano huo ulistawi, na kwa hila, alichukua udhibiti wa kampuni ya nguo iliyokuwa ikizorota, na kuibadilisha ikawa na mafanikio zaidi kifedha.

Hatua baada ya hatua, utajiri wake uliongezeka, lakini alibaki imara, maisha yake ya kawaida yakiwa ushuhuda kuwa kanuni zake hazikubadilika.

Wakati ulimwengu ulipoanza kuuliza bingwa huyu wa uwekezaji ni nani, tayari alikuwa bilionea kwa juhudi zake mwenyewe. Haikuwa mwingine ila Warren Buffett, Bingwa wa Omaha.

Je, kwa nini ninakupa hadithi hii? Mwanzoni mwa makala haya, nilizungumza kuhusu hali isiyo ya kawaida ambayo hufanya trader mmoja kuwa bora zaidi kuliko mwingine.

  1. mtazamo au tabia maalum 

  2. elimu sahihi 

  3. bahati ya kawaida na rahisi

  4. pesa kutengeneza pesa

Warren Buffet alikuwa na mtazamo sahihi tangu mwanzo, hiyo ni hakika. Tabia na matamanio yake yalimfanya atafute elimu sahihi, hata majaribio ya awali yalipokosa kufaulu. Elimu aliyopata ilimsaidia kutambua uwezo mkubwa wa kampuni ya nguo ya New England iliyokuwa ikizorota wakati wengine hawakuweza kutambua hivyo. Wengine wanasema kuwa alibahatika, lakini watu wengi waliofanikiwa husema kuwa wanatengeneza bahati yao wenyewe.

Berkshire Hathaway ikawa inatengeneza pesa, ambapo Buffet alijenga himaya na kupata thamani ya zaidi ya bilioni $121 (USD), na alifanya hivyo kutokana na kuwa na vipengele vyote vinne vya mafanikio. Lakini hakuanza na vyote. Hapo awali, alikuwa na mtazamo sahihi pekee, na ukamsaidia kupata vile vingine vitatu.

Kwa hivyo, ninauliza tena: je, biashara inakufaa, na unafaa kwa biashara? Ikiwa una mtazamo unaofaa, ni wakati wa kuanza kujifunza, na njia bora ya ‘kujifunza’ ni ‘kufanya.’ Na kwa usaidizi wa Exness wa 24/7 na nyenzo za kielimu unazoweza kufikia, unahitaji muda na jicho pekee ili kuona fursa unazoweza kuchukua. Mabadiliko huanza ndani.


Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio ubashiri wa matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya trade kwa kuwajibika.


Mwandishi:

Paul Reid
Paul Reid

Paul Reid ni mwandishi wa habari za kifedha aliyejitolea kufichua miunganisho ya kimsingi iliyofichwa ambayo inaweza kuwapa traders faida. Akilenga zaidi soko la hisa, hisia za Paul za kutambua mabadiliko makubwa ya kampuni zimethibitishwa vyema kutokana na kufuata masoko ya kifedha kwa zaidi ya muongo mmoja.