Maarifa

Kwa nini traders wa dhahabu wanapaswa kuangazia USOIL

Na Paul Reid

14 Mei 2024

Trading gold

Traders wa XAU wamekuwa wakikabiliana na volatility kwa muda wa miezi michache iliyopita, huku bei ikishuka hadi $1,820 (USD), kupanda kwa viwango vipya vya juu wiki chache baadaye. Orders zilizoratibiwa vyema katika mwelekeo unaofaa kwa hakika ziliwafurahisha traders wachache wa XAU mwaka huu, lakini ikiwa kwa sasa huna order iliyofunguliwa ya dhahabu chini ya 1900, unaweza kuwa na kikomo cha volatility ya sasa ya trade ya mchana.

Kinyume chake, USOIL imekuwa ikifaidi traders mara kwa mara, licha ya volatility ya kisiasa na kiuchumi kuathiri kila soko. Kwa mabadiliko ya muda mfupi na ya muda mrefu, wawekezaji na traders wa mchana wana options nyingi. Lakini je, biashara ya mafuta ni rahisi, hatari, au labda ni ya traders wenye uzoefu pekee?

Unaweza kushangaa kujua kwamba hauitaji hata kujua uchanganuzi wa kiufundi ili kutrade mafuta. Hebu tujue ni kwa nini.

USOIL - mali ya traders wote

USOIL inafaa kwa traders wa viwango vyote. Isitoshe, unaweza kuvinjari hatua za bei ya mafuta bila hata kutumia zana za kimsingi za kiufundi. Hebu tuangalie chati na tuone kwa nini traders wa mikakati yote huchagua USOIL.

Mienendo ya bei

Kuna mwenendo thabiti unaoweza kubashirika ambapo bei inapanda na kushuka kwa haraka kisha inapanda tena. Ukifungua chati ya USOIL kwenye kivinjari chako, utaona mienendo mara moja. Ni mchoro unaonyesha kupanda na kushuka kwa bei ndani ya safu fupi ya bei.

Mabadiliko madogo na thabiti ya bei yako karibu na $4 hadi $6 kuanzia juu hadi chini, ambayo hutokea kila siku iwe ni mwenendo wa kupanda au kushuka.

Kisha kuna mabadiliko ya kati ya karibu $9 hadi $16, ambayo pia ni muhimu kwa hatua za bei zinazopanda na kushuka. Kwa traders ambao wangependa kununua kwa bei ya chini, kushikilia, na kuuza kwa bei ya juu, mabadiliko ya kati hutokea, kwa wastani, mara moja baada ya kila wiki 2.

Kuna mwenendo mwingine ambao hutokea mara chache, na kwa kawaida huwa ya kusisimua. Hii inafaa zaidi kwa trader wa muda mrefu ambaye angependa tu kununua kwa kwa bei ya chini na kushikilia, au kununua kwa bei ya juu na kusubiri. Katika kipindi cha miaka 5 iliyopita, USOIL imekuwa na trend ya jumla ya kupanda kwa mara kadhaa, ambayo huwekwa upya ghafla. Uwekaji upya huu mkubwa unaweza kupunguza bei kwa hadi $50. Mtu yeyote anayejaribu kuuza mafuta wakati wa mizunguko hiyo anaweza kupata faida kubwa, lakini traders wa trend wanaofuata mwenendo wa kupanda polepole hupata hasara. 

Ni ngumu sana kubashiri mienendo hii lakini hutoa matokeo makubwa zaidi. Haya hubashirika vyema kwa kutumia habari za msingi za soko kama vile kupunguzwa kwa uzalishaji katika OPEC au masuala ya usambazaji na mahitaji.  Kumbuka tu kwamba mara nyingi kuna hisia ndogo na ya papo hapo ya habari ikifuatiwa na mwitikio mkubwa unaofuata baada ya wiki kadhaa. Katika biashara.

Ikiwa unatarajia kufaidika na mojawapo ya hatua kubwa za bei, labda utahitaji kununua na kushikilia, ikiwezekana kwa miezi kadhaa. Angalia chati sasa ili kuona zamu ya mwisho kubwa ilifanyika lini. Labda ingine iko karibu kutokea.

Jinsi ya kutrade ya mafuta kila siku/wiki?

Mkakati usioratibiwa vizuri hauna manufaa yoyote. Hebu tuchunguze mkakati, lakini itabidi uratibu points za kuingia vizuri ili upate manufaa kamili ya volatility ya mafuta.

Angalia chati sasa hivi. Weka timeframe kuwa saa 4 (upande wa juu kushoto wa chati), na aikoni moja upande wa kulia itabadilika kutoka kwa vinara hadi line. Sasa utaona hatua za kupanda na kushuka za bei. Pia utaona sehemu ambapo bei inabaki kuwa sawa, na mara kwa mara, hatua kubwa ya bei. Hebu tuangalie upande wa kulia wa chati na tuone kinachotokea sasa hivi.

Je, bei ya sasa inashuka au inapanda? 

Bei ya kushuka chini

Fuatilia hadi kilele cha mwisho na uangalie bei. Ikiwa tabia ya bei itasalia kuwa thabiti, huenda mojawapo ya hatua tatu za bei inaendelea. Hatua ya bei ya chini, hatua ya bei ya kati, au mabadiliko makubwa ya muda mfupi. Moja kati ya hizo inaanza.

Fuatilia bei kutoka kilele cha mwisho na ubashiri mahali ambapo mabadilko madogo na ya kati yanaweza kutokea. Hizo zinaweza kuwa points ambapo unaweza kuingilia. Unapoona bei ikishuka kisha kuanza kupanda katika mojawapo ya points hizo zilizotarajiwa, unaweza kuwa unatazama mabadiliko yanayofuata.

Iwapo itabainika kuwa ni hatua ya bei ya muda mfupi inayoendelea, kila mtu anaweza kubashiri mahali bei itafikia, kwa hivyo ukipata order ya ununuzi katika point ndogo au ya kati, hakikisha kuwa unalinda funds zako kwa kutumia kipengele cha Exness cha stop loss.

Hatua ya bei ya kupanda

Ni nadra kuona ongezeko la bei la haraka kwa USOIL, lakini hutokea mara kwa mara. Ikitokea, basi order ya ununuzi ililowekwa vizuri itakuletea faida nzuri, lakini hebu tuzingatie hatua za bei za kawaida zaidi. Fuatilia hadi kwenye bei ya chini zaidi ya hivi majuzi na uongeze safu ndogo au ya kati ya mabadiliko. Hizo ni points mbili zinazowezekana za mabadiliko za kuzingatia.

Kwa mfano, ikiwa USOIL ina trend ya kupanda na inapita $82, hatua ndogo ya bei itafikia $88, ambayo inaweza kuwa point ya kuingilia ya uuzaji wa USOIL. Ikiwa safu ni hatua ya bei ya kati, itaendelea kupanda hadi karibu $95 kabla ya kufikia resistance.

Iwe inapanda au kushuka, lengo lako ni kutazama chati kwa urahisi na kusubiri mabadiliko yafanyike katika hatua ya bei ya chini au ya kati. 

Hitimisho

Iwe unajaribu tu kupunguza bei zinazopanda kwenye kituo cha mafuta au unafikiria kufanya USOIL kuwa instrument yako ya biashara ya kila siku/wiki, Exness ina kila kitu unachohitaji. Kutoka kwa vipengele vya ulinzi vinavyoweza kuzuia bei kushuka hadi gharama za chini za biashara ambayo huongeza faida inayoweza kupatikana wakati wa kupanda kwa bei.

Kama ilivyo kwa instruments zote maarufu za biashara, utahitaji kuwa mwangalifu, kwa hivyo hakikisha kuwa umesakinisha programu ya Exness Trade ili upate arifa za papo hapo za mabadiliko ya soko. Athari mpya zinaongezeka, kwa hivyo tunaweza kuona mabadiliko katika mitindo hii.

Hakikisha kuwa akaunti yako ya Exness inatumika na iko na funds ili uweze kutrade bila kuchelewa, lakini kuwa na subira na usubiri hadi imani yako iwe ya juu kabla ya kufanya biashara. Iwapo ulikosa fursa, usifuate ya jana… kila mara kuna nyingine itakayotokea hivi karibuni, na ukiwa na USOIL, hutahitaji kusubiri kwa muda mrefu.


Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio ubashiri wa matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya trade kwa kuwajibika.


Mwandishi:

Paul Reid
Paul Reid

Paul Reid ni mwandishi wa habari za kifedha aliyejitolea kufichua miunganisho ya kimsingi iliyofichwa ambayo inaweza kuwapa traders faida. Akilenga zaidi soko la hisa, hisia za Paul za kutambua mabadiliko makubwa ya kampuni zimethibitishwa vyema kutokana na kufuata masoko ya kifedha kwa zaidi ya muongo mmoja.