Kuhusu Kalenda ya Kiuchumi
Kalenda ya Kiuchumi ni kipengele kinachosaidia wafanyabiashara kufuatilia na kuchanganua matukio ya soko, na kubashiri mienendo zaidi ya bei. Inaangazia habari zijazo za kitaifa na kimataifa kote ulimwenguni kwa mpangilio kulingana na tarehe.
Matukio haya makuu yanaweza kuwa na athari kubwa kwenye masoko ya fedha na kwa kawaida hutangazwa au kutolewa katika ripoti. Mifano ya matukio kama haya ni pamoja na maamuzi ya sera za fedha, indicators za kiuchumi, matangazo ya Pato la Taifa (GDP), nambari za Malipo ya Mashirika Yasiyo ya Kilimo (NFP), maamuzi ya viwango vya riba na mengine mengi.
Huwa tunawaarifu wafanyabiashara kabla ya matukio, habari na matoleo ya data yajayo ili kuwafahamisha kuhusu saa na instruments ambazo zinaweza kuathiriwa. Unaweza kupata arifa hizi chini ya kichupo cha "Mailbox" kwenye jukwaa lako la biashara. Tafadhali kumbuka kuwa athari za habari za kiuchumi na indicators zinaweza kutofautiana kwa kila instrument.