Usalama wa akaunti na ulinzi wa mteja

Tumejitolea kutoa mazingira salama ya biashara, kwa usalama wa akaunti ulioimarishwa, ulinzi wa fund na huduma wa mteja ya 24/7 ili iwe rahisi kwako.

Tunaelewa wasiwasi wa ulaghai wa uwekezaji na hatari kwa traders, ndiyo maana amani yako ya kiakili ndiyo kipaumbele chetu kikuu. Katika Exness, utanufaika kutokana na hatua za kisasa za usalama ili kuhakikisha kwamba akaunti yako, taarifa za kifedha na maelezo yako ya kibinafsi yanaendelea kulindwa kila wakati. Kuanzia teknolojia za hali ya juu za usimbaji fiche hadi itifaki kali za uthibitishaji, tunaendelea kujitahidi kudumisha viwango vya juu zaidi vya usalama wa akaunti ili uweze kutrade kwa ujasiri.

Tuko hapa kwa ajili yako

Kama broker anayeongoza duniani aliye na leseni na anayedhibitiwa, tunakupa options nyingi za usalama wa akaunti kwa biashara salama.

Sheria

Ikiwa umekuwa ukijiuliza, 'Je, Exness ni halali?', tunakuhakikishia kwamba sisi ni broker aliyeidhinishwa, anayedhibitiwa na mashirika ya kimataifa ya kiwango cha juu duniani kwa biashara salama.


Usalama wa akaunti kwa biashara salama

Zuia ufikiaji usioidhinishwa ili kulinda akaunti zako za kutrade kwa kuchagua option ya usalama – nambari ya simu au barua pepe – wakati wa mchakato wako wa usajili.

Ulinzi wa jukwaa kwa biashara salama

Pata maelezo zaidi kuhusu masharti yetu ya biashara salama na hatua za ulinzi ili kufanya biashara bila hitilafu.

Ulinzi dhidi ya shambulio la tovuti kwa biashara salama

Programu yetu ya Wavuti ya Kingamtandao (WAF) hulinda miundombinu na seva zetu dhidi ya hatari za wavuti kama vile kuathiriwa na SQL, mashambulizi ya XSS, na kuzuia trafiki hatari kwa biashara salama.


Uwezo wa kukabiliana na hitilafu za jukwaa la biashara

Ulinzi wetu wa dhidi ya DDoS hukupa biashara salama kupitia execution bila hitilafu, ufikiaji wa 24/7 wa Eneo lako la Binafsi, hatua za haraka za uwekaji na utoaji fedha, na shughuli za seva zisizokatizwa.


Mbinu ya kuthibitisha kila wakati

Muundo wetu wa Kuthibitisha kila wakati hupunguza uaminifu kwa vipengele vya kiteknolojia vya kampuni na hujumuisha vipengele kama vile uthibitishaji wa mtumiaji na kifaa, ufikiaji wenye vikwazo, na ufuatiliaji wa mtandao kuwezesha biashara salama.


Programu ya Zawadi kwa Kutambua Hitilafu

Kwa biashara salama, unapata usalama wa ziada kwa programu yetu ya Zawadi kwa Kutambua Hitilafu, ambapo tunawaalika wataalamu kutoka nje kuchunguza mifumo yetu na kutoa maoni ambayo yanatusaidia kuboresha huduma zetu.


Maarifa na ujuzi wa usalama mtandaoni

Timu yetu ya Usalama wa Taarifa hupata habari mpya mara kwa mara kuhusu teknolojia ya biashara salama na kuboresha ujuzi wao kupitia warsha na uthibitishaji.

Ulinzi wa malipo

Pata maelezo kuhusu vipengele vyetu mbalimbali vya biashara salama ya malipo vinavyolipiwa ili kulinda transactions zako za malipo.

Utoaji fedha kwa urahisi

Kipengele chetu cha utoaji fedha kiotomatiki huhakikisha kwamba tunashughulikia maombi yako ya utoaji fedha papo hapo, na kukupa ufikiaji wa funds zako hata wakati wa wikendi. Kasi ya malipo hutegemea njia uliyochagua ya malipo.

Uthibitishaji Salama wa 3D

Tunahakikisha biashara salama kwa kutumia transactions za kadi ya usalama wa malipo ya 3D, inayotoa ulinzi wa ziada wa ulaghai kupitia pin ya mara moja iliyotumwa kwa simu yako.

Akaunti zilizotengwa

Tunalinda funds zako kwa kuziweka katika akaunti tofauti na funds zetu. Funds zetu huwa nyingi kila wakati, hivyo tunaweza kukidhi mahitaji yako ya utoaji fedha katika biashara salama wakati wowote wa siku.

Utiifu wa masharti ya PCI DSS

Tumekaguliwa kikamilifu, na kuzingatia masharti yote ya PCI DSS, kuhakikisha usalama wa data ya kadi na biashara salama kupitia usimamizi madhubuti, mipangilio maalum ya usalama na ukaguzi wa mara kwa mara wa uwezekano wa kuathirika.

Ulinzi wa biashara

Fanya biashara salama kwa faida zaidi ukitumia vipengele vyetu maalum vya ulinzi.

Ulinzi Dhidi ya Salio Hasi

Fanya biashara salama bila wasiwasi ukiwa na uhakika kuwa hutadaiwa pesa na broker wako; tunazuia hasara zisizidi salio lako katika aina zote za akaunti za kutrade.

Mazingira ya kuaminika ya biashara

Fanya trade bila kukatizwa huku teknolojia ya kisasa ikihakikisha uthabiti wa jukwaa, viwango vikubwa ya biashara, execution ya haraka na spreads thabiti hata wakati wa volatility ya juu.

Chukua hatua za kujilinda

Imarisha usalama wako kwa kupata maelezo kuhusu mbinu zinazosaidia kuzuia shughuli za akaunti zisizoidhinishwa, ulaghai na majaribio ya ulaghai.

Weka Eneo lako la Binafsi kuwa la faragha, usishiriki kamwe ufikiaji na hati za kibinafsi. Usiruhusu mtu yeyote atumie jina lako kufungua akaunti ya Exness au kushiriki maelezo yako ya usalama.


Fanya shughuli za kifedha ndani ya Eneo la Binafsi la Exness pekee na usihamishe pesa kwa akaunti zisizojulikana na hii huhakikisha biashara salama.


Ili kuhakikisha biashara salama, jihadhari na viungo vinavyotiliwa shaka na vyanzo visivyojulikana, usitoe kamwe taarifa nyeti unapopokea mawasiliano bila kutarajia, na uwasiliane moja kwa moja na Exness kupitia gumzo ya moja kwa moja au utume barua pepe ukiwa na wasiwasi wowote kuhusu shughuli za ulaghai au uhalali wa ujumbe.

Maswali yanayoulizwa sana

Exness ni broker wa kimataifa aliyedhibitiwa vyema, aliyepewa leseni na mashirika kadhaa ya usimamizi ya kimataifa ili kuhakikisha usalama wa kifedha wa wateja wake. Kampuni hii ina idhini kutoka kwa Mamlaka ya Huduma za Kifedha (FSA) nchini Ushelisheli, Benki Kuu ya Curaçao na Sint Maarten (CBCS), Tume ya Huduma za Kifedha (FSC) katika Visiwa vya Virgin vya Uingereza na Mauritius, Mamlaka ya Maadili ya Sekta ya Kifedha (FSCA). nchini Afrika Kusini, Tume ya Dhamana na Ubadilishaji fedha ya Kupro (CySEC), Financial Conduct Authority (FCA) nchini Uingereza, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji (CMA) nchini Kenya na Tume ya Dhamana ya Yordani (JSC). Mashirika haya ya udhibiti yanasimamia shughuli za Exness katika maeneo ya mamlaka husika, kwa lengo la kudumisha uadilifu, uthabiti na usalama wa sekta ya huduma za kifedha. Hata hivyo, Exness haitoi huduma kwa wakazi wa maeneo fulani ya mamlaka, ikiwa ni pamoja na Marekani.

Exness inachukuliwa kama jukwaa salama la biashara, kwa mujibu wa hali yetu kama broker aliye na leseni na anayedhibitiwa na mashirika maarufu ya udhibiti ya kimataifa. Tunapea usalama wa akaunti kipaumbele kwa kutoa hatua mbalimbali za usalama kama vile uthibitishaji wa simu au barua pepe, ulinzi wa hali ya juu dhidi ya uvamizi wa tovuti kwa kutumia Programu ya Kinga ya Tovuti (WAF), na ulinzi wa DDoS ili kuhakikisha kuwa operesheni za biashara zinaendelea vizuri. Kampuni hii hutumia mbinu ya Kuthibitisha Kila Wakati kwa usalama wa IT, huendesha programu ya Zawadi kwa Kutambua Hitilafu ili kutambua udhaifu unaowezekana, na kusasisha maarifa ya usalama wa mtandao ya timu yake. Zaidi ya hayo, Exness hutumia vipengele vya ulinzi wa malipo, ikiwa ni pamoja na akaunti zilizotengwa na uthibitishaji wa 3D Secure, na hutoa ulinzi wa biashara kama vile Ulinzi dhidi ya Salio Hasi, kuhakikisha kuwa wateja wanaweza kutrade kwa ujasiri na wana amani ya kiakili.

Akaunti za Exness ina aina mbalimbali za usalama za kuthibitisha utambulisho wa mmiliki wa akaunti na kulinda taarifa nyeti. Aina hizi za usalama ni pamoja na simu, barua pepe na TOTP (inapatikana katika nchi fulani pekee). Kila hatua ya akaunti inahitaji msimbo wenye herufi sita, unaotumwa kwa aina ya usalama iliyochaguliwa, ili kuwekwa kama uthibitisho. Ni aina moja tu ya usalama inayoweza kutumika kwa wakati mmoja, lakini mabadiliko yanaweza kufanywa chini ya masharti fulani. Pia, PIN ya kipekee ya Usaidizi yenye herufi na nambari hutolewa ili kufanya kazi kama kiwango cha juu zaidi cha usalama. PIN hii hutumika kuthibitisha mmiliki wa akaunti wakati unawasiliana na usaidizi, na kuhakikisha kuwa maelezo nyeti yanafikiwa na mmiliki halisi wa akaunti pekee.

Hapana, Exness ni halali. Exness ni broker anayeheshimika wa mtandaoni wa mali nyingi aliyeanzishwa mwaka wa 2008 na kusajiliwa rasmi na kudhibitiwa na mamlaka mbalimbali za kifedha duniani kote.

Mbali na mfumo wake dhabiti wa udhibiti, Exness hupa usalama wa mteja kipaumbele kwa kutekeleza hatua dhabiti za ulinzi. Traders wanaweza kuwa na ujasiri katika usalama wa akaunti zao na uadilifu wa transactions zao kwa mujibu wa itifaki za kisasa za usalama na mipango ya ulinzi wa fund. Kwa kuchagua Exness, unachagua mfumo wa kuaminika ambapo usalama wa uwekezaji wako na taarifa za kibinafsi unashughulikiwa kwa umuhimu mkubwa, kuhakikisha uzoefu wa biashara unaotegemewa na salama.

Aina za kawaida za ulaghai ni pamoja na ulaghai wa kulipa ada mapema, ulaghai wa kununua hisa zisizo na thamani, ulaghai wa kupata mapato haraka au miradi ya piramidi, mitandao ya kijamii, crypto, forex, na ulaghai wa usambazaji wa taarifa za uwongo kuhusu hisa, huku wizi wa data ukiwa umeenea sana. Katika mashambulizi haya, wahalifu wa mtandao huiga udalali katika barua pepe ili kuiba maelezo yako ya kuingia na kufikia akaunti zako za kutrade. Kuna ishara kadhaa za onyo zinazoweza kukusaidia kutambua ulaghai. Kwa mfano, sarufi na tahajia duni, anwani za barua pepe na vikoa visivyolingana, hali ya dharura, viungo na viambatisho vinavyotiliwa shaka, mapato ya juu kuliko kawaida kwa biashara, shinikizo la kuchukua hatua haraka na mwingiliano na huluki ambazo hazijasajiliwa. Thibitisha usajili wa mtu binafsi au kampuni yoyote inayokuja na fursa za uwekezaji ili kulinda fedha zako kila wakati.

Kuwa mwangalifu unapojihusisha na biashara salama. Jilinde dhidi ya ulaghai kwa kutoshiriki maelezo nyeti kama vile manenosiri, vitambulisho au aina za usalama za Exness. Wawakilishi wa Exness hawaulizi kamwe taarifa kama hizo kupitia maandishi, barua pepe au mitandao ya kijamii. Usiache Maeneo yako ya Binafsi wazi, kufanya shughuli za Exness nje ya Maeneo ya Binafsi, au uhamishe pesa kwa akaunti zisizojulikana. Jihadhari na viungo visivyojulikana na usishiriki manenosiri. Ikiwa unashuku ulaghai, wasiliana na Exness mara moja kupitia live chat au barua pepe. Kuwa mwangalifu na jumbe za Exness zisizotarajiwa; ukiwa na shaka, wasiliana na usaidizi. Ikiwa umeshiriki maelezo ya faragha bila kukusudia, badilisha nenosiri lako mara moja.

Exness ni jukwaa halali la biashara ya mtandaoni, kwa kuwa limeidhinishwa na kudhibitiwa na mashirika kadhaa ya kimataifa ya udhibiti yanayoheshimiwa, kuhakikisha kwamba usalama wa kifedha wa mteja unalindwa. Kuwepo kwa leseni nyingi za udhibiti ni dalili tosha kwamba Exness inafanya kazi chini ya masharti makali.

Ili kuzingatia biashara salama, Exness hukaguliwa kipekee na inatimiza masharti yote ya PCI DSS (Kiwango cha Usalama wa Data ya Sekta ya Malipo) kwa malipo salama. Hii ni pamoja na usimamizi bora wa data, usalama maalum wa watoa huduma, usimbaji fiche wa data, ufuatiliaji wa mtandao, na ukaguzi wa mara kwa mara wa uwezekano wa kuathirika, na kuwalinda watumiaji dhidi ya uwezekano wa ukiukaji wa data na ulaghai wakati wa malipo ya kadi ya benki.

Fanya biashara na broker anayeaminika leo

Jionee mwenyewe kwa nini Exness ndiye broker anayefaa zaidi kwa traders zaidi ya 800,000 na washirika 64,000.