Hati za Kisheria
Pata maelezo yote unayohitaji kujua kuhusu mikataba yetu ya kisheria.
Matangazo
Septemba 9, 2024
Tungependa kuwajulisha wateja wote wa Exness (KE) Ltd kuwa hivi majuzi tulisasisha Mkataba wetu wa Mteja kama mojawapo ya juhudi tunazoendeleza za kuboresha utoaji wetu wa biashara na kuboresha vipengele muhimu vya uhusiano wetu na wateja wetu. Tunakuhakikishia kuwa Mkataba uliosasishwa wa Mteja hautaathiri operesheni zako za biashara na Exness (KE) Ltd.
Tunakuomba ukague Mkataba wa Mteja uliosasishwa na ikiwa una maswali yoyote, tutumie barua pepe kwa support@exness.ke. Timu yetu ya wataalamu wa Huduma kwa Wateja itakusaidia.
Tafadhali kumbuka kuwa hakuna hatua zaidi inayohitajika kwa upande wako kwa sasa, kwani Mkataba wa Mteja uliosasishwa utaanza kutekelezwa kiotomatiki baada ya siku tano (5) za kazi.
Asante kwa ushirikiano wako.
Tangazo muhimu
Machi 5, 2024
Tungependa kuwafahamisha wateja wetu kwamba Tadenex Ltd itakuwa ikifanya kazi kuanzia sasa chini ya jina jipya la Exness (KE) Ltd na kwa hali hii hati zetu zote za kisheria zimesasishwa ili kuonyesha mabadiliko hayo.
Desemba 12, 2023
Tafadhali fahamu kwamba kuanzia tarehe 12 Desemba 2023 (‘tarehe ya kuanza kutumika’), kiwango cha stop out cha akaunti zote za biashara kitaongezeka kutoka 0% hadi 20%. Kipengele cha sasa cha ulinzi cha stop out pia kitazimwa. Hii ina maana kwamba kuanzia tarehe 12 Desemba, orders zozote zilizo wazi zitafungwa kiotomatiki kiwango cha margin kinapofikia 20%. Hata hivyo, kumbuka, katika nyakati za volatility ya juu ya soko, kiwango cha margin kinaweza kushuka chini ya 20%. Mabadiliko yaliyotajwa hapo juu zitaathiri orders zozote ambazo zimefunguliwa, au kuwekwa kuanzia tarehe ya kuanza kutumika.