Unachoweza kufanyia biashara kwenye MT4
Katika Exness, unaweza kufurahia kufanya biashara ya CFD katika zaidi ya instruments 200, ambazo ni pamoja na kufanya biashara ya jozi za sarafu za forex, metali, hisa, fahirisi na nishati.
Forex
Kuna zaidi ya majozi 100 ya sarafu yanayopatikana kwa biashara ya CFD kwenye MT4 katika Exness. Tunatoa jozi za sarafu kuu, ikiwa ni pamoja na EURUSD, GBPUSD na USDJPY, na jozi za sarafu ndogo. Pia kuna orodha ndefu ya majozi nadra yanayopatikana kufanyia biashara ya CFD.
Metali
Katika MT4 ukitumia Exness, unaweza kufanya biashara ya CFD kwenye metali kwa njia ya jozi za sarafu, ambazo ni pamoja na XAUUSD, XAUEUR, XAUGBP na XAUAUD kwa dhahabu na XAGUSD, XAGEUR, XAGGBP na XAGAUD kwa fedha. Unaweza pia kufanya biashara kwa platinamu (XPT) na paladiamu (XPD) kwa jozi za sarafu.
Hisa, Fahirisi na Nishati
Kwa sasa, wafanyabiashara kwenye MT4 wanaweza kufanya biashara ya CFD kwenye zaidi ya hisa 80, ambazo zimeorodheshwa kwenye tovuti yetu, na fahirisi 10, ikiwa ni pamoja na US30, DE30, HK50, UK100, na AUS200. Kuhusu nishati, tunatoa CFD kwenye UKOIL na USOIL.