MetaTrader 5 (MT5)

Fanya biashara ya CFD kwenye instruments unazopendelea za biashara kwa kutumia MetaTrader 5. Jukwaa madhubuti la majozi ya sarafu na financial instruments zingine zinazofanya biashara ya CFD, MetaTrader 5 inaweza kupakuliwa kwenye Exness bila malipo.

Vipengele Vikuu vya MetaTrader 5

MetaEditor

Katika MetaTrader 5, unaweza kutengeneza roboti za biashara na indicators za kiufundi kupitia zana maalumu ya MetaEditor. Zana hii inapounganishwa na jukwaa, mipango mipya itaonekana kiotomatiki kwenye MetaTrader 5 yako na inaweza kutekelezwa papo hapo.

MetaQuotes Language 5

Lugha ya programu kwa mikakati ya biashara, MetaQuotes Language 5 (MQL5) inaruhusu uundaji wa hati, roboti za biashara na indicators. Uboreshaji wa MQL5 uliondoa mapungufu kadhaa ya toleo la awali, MQL4, hivyo basi kuongeza idadi ya vipengee na vifaa vya picha.

Mfumo wa Hedging

Katika MetaTrader 5 ukitumia Exness, unaweza kufanya biashara kwa kutumia muundo wa mfumo wa hedging. Hedging hukuruhusu kufungua positions nyingi, hata positions tofauti kabisa, kwa instrument ya biashara.

Chati na Muda

Fuatilia mienendo ya bei ya wakati halisi katika chati za vipindi vya dakika 1 hadi mwezi 1 na hadi vipindi 21 kwa wakati mmoja. Kipengele hiki huwaruhusu wafanyabiashara kujibu mabadiliko ya bei papo hapo, na pia kuhifadhi historia ya bei katika fomu iliyoshikamana.

Uchanganuzi wa Msingi

Pata fursa za soko kwa vifaa vya msingi vya uchanganuzi kwenye MetaTrader 5, kama vile Kalenda ya Kiuchumi ya ndani. Endelea kupata habari za hivi punde, athari za soko na ubashiri.

Indicators na Vifaa vya Uchanganuzi

Boresha hali yako ya utumiaji ya kufanya biashara kwa indicators 38 zilizojengewa ndani, vifaa 22 vya uchanganuzi na vifaa 46 vya picha unapofanya biashara ya financial instruments katika jukwaa la biashara.

Kuhusu MetaTrader 5

Toleo la tano la majukwaa ya MetaTrader, MetaTrader 5 hutoa utendaji na vipengele bora kuliko toleo la awali na kwa haraka likawa mojawapo ya majukwaa maarufu ya biashara na wafanyabiashara wa fedha za kigeni wa mtandaoni na huduma za wakala duniani kote.

Jinsi MetaTrader 5 Ilitengenezwa

Upeo wa biashara huanza kunapokuwa na zana mahiri na rahisi kutumia, na kampuni ya programu ya MetaQuotes hutoa huduma kwa jukwaa la MetaTrader 5, kituo bora cha biashara kwa wafanyabiashara wa aina na viwango vyote vya ujuzi.

Iliyozinduliwa mwaka wa 2010 na kampuni ya maendeleo ya programu ya biashara ya fedha, MetaTrader 5 imezidi kuwa maarufu zaidi kati ya wafanyabiashara, mawakala na wale wanaotoa huduma za uwekezaji au mawakala.

Toleo linalofuata kufuatia mafanikio ya MetaTrader 4, jukwaa la mali nyingi lilikidhi mahitaji ya wafanyabiashara kwa kutoa sio tu biashara ya sarafu, lakini pia biashara kwa karibu masoko yote ya kifedha, ikiwa ni pamoja na soko la futures.

Matumizi ya MetaTrader 5

Uchambuzi wa kimsingi na wa kiufundi, ishara za biashara, biashara ya algoriti - jukwaa la biashara hutoa safu ya vifaa vinavyoboresha uzoefu wa biashara. Jukwaa pia lina utangazaji wa ripoti za hivi punde za habari za kifedha kwa wafanyabiashara kuwasasisha kuhusu masoko.

Kwa mawimbi ya biashara na uwezo wa kufanya biashara wa kunakili katika MetaTrader 5, wafanyabiashara wanaweza kufuata ishara za wafanyabiashara waliofaulu na kunakili mikakati na orders zao za biashara, ambayo yatatolewa kiotomatiki kwenye akaunti yako.

Biashara ya Kiotomatiki na MQL

Biashara ya kiotomatiki inawezekana kwenye MT5, kwa kutumia roboti za biashara, au Washauri Wataalamu, ambao huchanganua makadirio ya bei na kufanya shughuli kwenye masoko ya kifedha. Kuna indicators za kiufundi zilizosakinishwa awali na roboti za biashara kwenye jukwaa, lakini wafanyabiashara wanaweza kusakinisha zaidi au kutengeneza Washauri Wataalamu wao wenyewe kwa kutumia lugha ya programu, MetaQuotes Language 5 (MQL5).

Kufanya Biashara kwa Simu na MetaTrader 5

Kituo cha biashara sio tu cha maeneokazi ya Windows, macOS na Linux. Wafanyabiashara walio na ratiba nyingi wanaweza pia kufanya biashara kutumia simu kwenye simu mahiri na kompyuta vibao za iOS na Android. Ukiwa na zana zote muhimu za biashara, ikiwa ni pamoja na orders za biashara, chati shirikishi na zana maarufu za uchanganuzi, unaweza kufuatilia akaunti yako na kufanya biashara ya simu kwa kubofya mara moja.

Jukwaa lenye Uwezo la Vipengee Vingi

Kituo cha Biashara cha Kompyuta ya Mezani cha MT5

  • Zaidi ya instruments 200 za biashara
  • Madarasa 6 ya mali
  • Aina 5 za akaunti za biashara
  • Spreads za chini hadi 0.0
  • Ada kuanzia 0
  • Aina 8 za pending order (Buy Stop, Sell Stop, Buy Limit, Sell Limit, Take Profit, Stop Loss, Buy Stop Limit, Sell Stop Limit)
  • Muda 21 na aina 3 za chati
  • Inapatikana katika Windows, macOS and Linux
  • Instant execution na market execution
  • Mfumo wa Hedging
  • Indicators 38 zilizojengewa ndani na vifaa 22 vya uchanganuzi
  • Kalenda ya ubadilishanaji wa fedha za kigeni iliyojengwa ndani
  • Quotes za kiwango cha 2 zinatumika
  • Trailing stop, uchanganuzi wa kiufundi, na Indicators maalum, Washauri Wataalamu (EA) na Hati

Unachoweza kufanyia biashara kwenye MT5

Katika Exness, unaweza kufurahia kufanya biashara ya CFD katika zaidi ya instruments 200, ambazo ni pamoja na kufanya biashara ya jozi za sarafu za forex, metali, hisa, fahirisi na nishati.

Forex

Kuna zaidi ya majozi 100 ya sarafu yanayopatikana kwa biashara ya CFD kwenye MT5 katika Exness. Tunatoa jozi za sarafu kuu, ikiwa ni pamoja na EURUSD, GBPUSD na USDJPY, na jozi za sarafu ndogo. Pia kuna orodha ndefu ya majozi nadra yanayopatikana kufanyia biashara ya CFD.

Metali

Kwenye MT5 ukitumia Exness, unaweza kufanya biashara ya CFD kwenye metali kwa njia ya jozi za sarafu, ambazo ni pamoja na XAUUSD, XAUEUR, XAUGBP na XAUAUD kwa dhahabu na XAGUSD, XAGEUR, XAGGBP na XAGAUD kwa fedha. Unaweza pia kufanya biashara kwa platinamu (XPT) na paladiamu (XPD) kwa jozi za sarafu.

Hisa, Fahirisi na Nishati

Kwa sasa, wafanyabiashara kwenye MT5 wanaweza kufanya biashara ya CFD kwenye zaidi ya hisa 80, ambazo zimeorodheshwa kwenye tovuti yetu, na fahirisi 10, ikijumuisha US30, DE30, HK50, UK100, na AUS200. Katika nishati, tunatoa CFD kwenye UKOIL na USOIL.

Jinsi ya kufungua akaunti ya MT5 na Exness

Kabla ya kuanza kufanya biashara, fungua kwanza akaunti ya Standard au ya Professional ya MT5 ukitumia Exness. Baada ya usajili wa akaunti kufanikiwa, utaweza kupata maelezo ya akaunti yako ya MT5 yaliyoorodheshwa katika Eneo lako la Kibinafsi.

Jinsi ya kuingia kwenye akaunti ya MT5

Kwa Windows, macOS na Linux:
  • Anzisha kituo cha biashara kwenye Kompyuta yako
  • Kwenye kituo, bofya 'File' kisha uchague 'Login to Trade Account'
  • Kisha, weka nambari ya akaunti yako kama maelezo ya kuingia, nenosiri la biashara ya akaunti yako na seva ambayo akaunti yako ilisajiliwa
  • Baada ya kuingia, utasikia sauti ya kengele ikithibitisha kuingia kwako

Maswali yanayoulizwa sana

Pata majibu kwa maswali yanayoulizwa sana kuhusu kutumia MetaTrader 5.

Kwa kituo cha kompyuta ya mezani cha MetaTrader 5, utahitaji kuingia kwenye akaunti yako ya biashara. Ili kuingia:

  • Bofya 'File' na kisha ‘Login to Trade Account’

  • Weka maelezo ya kuingia, Nenosiri na Seva (maelezo ya kuingia na seva yanaweza kupatikana kwenye akaunti yako ya biashara katika Eneo la Binafsi huku nenosiri lako likiwa sawa na uliloweka kwa akaunti yako ya biashara)

  • Baada ya kuingia, utasikia sauti ya kengele ikithibitisha kuingia kwako na unaweza kuanza kufungua biashara.

Kwa miongozo ya jinsi ya kuingia katika mifumo mingine ya MetaTrader 5 kwenye Exness, tembelea Kituo chetu cha Usaidizi.

Mara tu unapofungua akaunti yako ya biashara ya MT5, unaweza kuweka agizo jipya la CFD katika jozi za sarafu, metali na instruments zingine nyingi. Kwa kituo cha kompyuta ya mezani cha MetaTrader 5:

  • Fungua agizo jipya kwa kubofya 'New Order' kwenye upau wa vidhibiti au kubofya mara mbili kwenye jozi ya sarafu ya fedha za kigeni unayotaka kwenye dirisha la 'Market Watch'

  • Baada ya kuchagua ishara, weka kiasi chako, stop loss na take profit

  • Kisha chagua ‘Market Execution’ au ‘Pending Order’

  • Kisha, bofya kwenye ‘Sell by Market’ au ‘Buy by Market’ ili kufungua biashara.

Unaweza kufunga order kwa kubofya order yako mara mbili na kubofya kitufe cha ‘Close by Market’ au kwa kubofya upande wa kulia wa order yako na kuchagua ‘Close Order’.

Majukwaa mengine ya MetaTrader 5 yanaweza kuwa na njia tofauti kidogo za kufungua biashara, ambazo unaweza kuzitazama katika Kituo chetu cha Usaidizi.

Huku ikiwa imeundwa na MetaQuotes, MetaTrader 5 sio tu maarufu kwa zana na vipengele vyake, lakini pia kwa usalama wake. Mfumo wa MT5 husimba kwa njia fiche data yote inayotumwa kati ya wafanyabiashara na seva za jukwaa, na kuhakikisha kuwa akaunti zako za biashara, miamala na data zinalindwa.

MetaTrader 5 hailipishwi. Exness haitozi ada yoyote kwa kupakua au kutumia chaguo zozote tofauti za jukwaa. Hata hivyo, muunganisho wa Intaneti wa kutumia kituo cha biashara na ada zingine zinazohusiana ni wajibu wa mfanyabiashara.