Maarifa

Matukio ya mdororo wa uchumi na mafuta ghafi

Na Paul Reid

10 Januari 2024

recession and oil 2024

Kwa miongo kadhaa, kuna uwezekano kwamba traders wa mdororo wa uchumi wa mafuta wanatambua kuwa mafuta yanaweza kuleta faida na pia hasara, wakisimulia hadithi kuu za mabadiliko ya usambazaji na mahitaji. Kwa zaidi ya mara moja, mafuta ghafi yamekuwa sababu ya kuanguka wa uchumi. Na huku kukiwa na mizozo na minong'ono ya mdororo wa uchumi katika mwaka wa 2024, mtu anaweza kushangaa kama tunaweza kutarajia mafuta kuwa na mienendo inayoweza kubashirika au la. Hebu turudi nyuma na tuone jinsi mafuta yalivyoathirika katika vipindi vya mdororo wa uchumi vilivyopita.

Mdororo wa uchumi wa mafuta ulianza katika miaka ya 1920, wakati wa kuongezeka kwa kutokuwa na usawa wa kiuchumi. Ulimwengu ulipokaribia Great Depression (1929-1939), mafuta yalikuwa mengi, soko lilikuwa thabiti, na bei zilikuwa kati ya $1.00 (USD) na $1.50 kwa kila pipa. Lakini Mdororo Huo ulipoendelea kushika kasi, uthabiti huo uliporomoka. Kufikia 1931, bei ilikuwa imeshuka chini ya $1 kwa kila pipa, ikifuatiwa na urejeshaji wa muda mrefu na unaobadilika-badilika. Bei ya mafuta haikuendelea vizuri kutokana na athari za mdororo wa uchumi za wakati huo.

Kusonga mbele hadi miaka ya 1970, muongo uliokumbwa na mzozo wa mafuta wa 1973/74. Hapa, hali ilibadilika. Kabla ya mdororo wa uchumi, bei ya mafuta ilikuwa kati ya $3 hadi $4 kwa kila pipa. Lakini mivutano ya kisiasa ya kijiografia iliyoibuka kutoka Mashariki ya Kati, hasa vikwazo vya mafuta vya Waarabu vya 1973, vilipelekea bei kupanda hadi $12 kwa kila pipa, na kuchochea mzozo wa kiuchumi duniani.

Baada tu ya ulimwengu kurejea kwa hali ya kawaida, bei ya mafuta ilipanda na kufikia bei ya juu zaidi katika mwaka wa 1980 kutokana na Mapinduzi ya Irani na vita vya Iran-Iraq. Bei ya mafuta ilipanda kutoka $14 hadi $39 kwa kila pipa katika mwaka wa 1979, lakini mdororo wa uchumi ulipoendelea, mahitaji yalipungua, na bei ikaanza kupungua.

Migogoro pia ilisababisha mdororo wa miaka ya mwanzo ya 1990. Kabla ya wakati huo, bei ya mafuta ilikuwa ikipanda polepole na kubadilika-badilika. Katika miezi iliyotangulia mdororo huo, bei ya mafuta ilikuwa imeshuka kutoka kwa bei ya juu kwa miaka 5 ya $22 hadi $17. Kisha, miezi miwili kabla ya vita hivo kuanza, bei ya mafuta ilipanda tena. Ndani ya miezi mitatu, bei ya mafuta iliongezeka zaidi ya maradufu hadi bei ya juu ya $39.51, lakini kiwango hicho cha juu kilikuwa cha muda mfupi. Miezi mitano baadaye, bei ilishuka hadi kati ya $20 na $25.

Kwa hivyo, kushuka kwa bei kabla ya mdororo wa uchumi, kupanda mwanzoni, na marekebisho ndani ya mwaka wa kwanza.

Kupanda na kushuka katika karne mpya

Tunapoingia katika karne ya 21, tunaanza na mdororo wa uchumi usiohusiana na mzozo wa Mashariki ya Kati — kushuka kwa bei ya stock kwa makumpuni mengi ya mtandaoni. Bei ya mafuta ilishuka kidogo kabla ya mdororo wa mwaka wa 2001, huku ikipanda kidogo kutoka $26 hadi $28 na ulimwengu wa kifedha ukikubali kuwa mdororo wa uchumi ulikuwa unaendelea. Mwezi mmoja kabla ya mkasa wa 'Septemba 11' ulioshtua ulimwengu, bei ya mafuta ilishuka na kuendelea kushuka hadi Novemba, ilifikia bei ya chini ya $ 19.

Bei ilishuka kidogo kabla ya mdororo wa uchumi, na kufuatiwa na kushuka kwa kiwango kikubwa.

Kufikia 2007, tulishuhudia kupanda kwa bei ya mafuta. Mnamo Aprili, mtoa huduma maarufu wa rehani aliwasilisha ripoti ya kufilisika, huku mnamo Juni, hedge funds mbili kuu zilikabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha. Matukio haya yalikuwa kwenye habari, lakini hakuna mtu aliyeshuku chochote wakati huo.

Soko la hisa lilifikia bei za juu zaidi mnamo Julai 2007, na bei ya mafuta iliendelea kupanda. Kisha, bodi ya Fed iliingilia kati, na kuongeza liquidity kwenye mfumo wa benki na, baadaye katika mwaka huo, ilianza kupunguza kiwango cha riba. Mambo yote yaliharibika kuanzia hapo, lakini bei ya mafuta iliendelea kupanda hadi Juni 2008. 

Kisha ikashuka, ikishuka kutoka bei ya juu ya $140 hadi $41 katika muda wa miezi sita pekee. Mtu yeyote aliyekuwa na position ya ununuzi kwenye mafuta alikuwa na uhakika kuwa angepeta hasara kubwa. Bei kupanda kabla ya mdororo wa uchumi, kisha mabadiliko ya kiwango kikubwa.

Mambo muhimu ya kutajwa

Ingawa 2014 haihesabiwi rasmi kuwa na mdororo wa uchumi, bei ya mafuta ilishuka sana kutoka $105 hadi $48 mwaka huo. Hiyo ilikuwa ni kwa sababu Marekani ilikuwa imeongeza uzalishaji wa mafuta kwa kiasi kikubwa kutokana na maendeleo ya kiteknolojia katika upasuaji wa miamba kwa kutumia majimaji yenye shinikizo la juu, inayojulikana kama 'fracking' na kuchimba visima vilivyolala, na hivyo kuongeza uzalishaji wa mafuta yanayotoka kwenye mawe. OPEC ilibahatisha na haikupunguza uzalishaji, na kusababisha usambazaji kupita kiasi kwa kiwango kikubwa. 

Tatizo kama hilo lilitokea tena mnamo 2019/2020 wakati tasnia na masoko ya ulimwengu yalisitisha kazi kutokana na COVID.

Hitimisho

Muda baada ya muda, tumeona mwaka ambao bei inabadilika-badilika lakini kuna mwenendo wa kupanda ukitangulia mdororo wa uchumi. Miezi kabla ya tarehe rasmi za mdororo wa uchumi ilionyesha bei ikishuka kidogo, kisha ikafuatiwa na kupanda kwa bei kwa kiwango kikubwa. Na mara nyingi sana, kupanda huko kwa bei kuliisha ghafla, ikifuatiwa na kushuka kwa bei kwa kiwango kikubwa.

Kuhusu muda wa matukio haya, ni rahisi kuangalia nyuma na kuona sehemu zinazofaa za kuingilia na kutoka, lakini kuangalia mwonekano wa kila siku kunaweza kuonyesha volatility muhimu ambayo huenda iliathiri akaunti nyingi za kutrade.

Iwapo unapanga kutrade mafuta kabla ya mdororo wa uchumi uliobashiriwa wa 2024, hakikisha kuwa umechagua leverage yako kwa uangalifu na ujitayarishe kwa kushuka kwa bei kwa kuweka stop loss. Kuhusu kuweka take profit, kulenga juu sana kunaweza kukuathiri, kwa hivyo kuwa na matarajio ya kawaida ya faida.


Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio ubashiri wa matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya trade kwa kuwajibika.


Mwandishi:

Paul Reid
Paul Reid

Paul Reid ni mwandishi wa habari za kifedha aliyejitolea kufichua miunganisho ya kimsingi iliyofichwa ambayo inaweza kuwapa traders faida. Akilenga zaidi soko la hisa, hisia za Paul za kutambua mabadiliko makubwa ya kampuni zimethibitishwa vyema kutokana na kufuata masoko ya kifedha kwa zaidi ya muongo mmoja.