Pip calculator ya biashara

Kokotoa pips kutumia pip calculator, margin, spread, ada na zaidi ukitumia kikokotoo cha uwekezaji cha Exness. Zana yetu muhimu inaweza kukusaidia kurahisisha ukokotoaji changamano kwa trading positions zako.

Order yako
Matokeo
Margin
Gharama ya spread³
Ada
Swap short
Swap long
Thamani ya pip

Kanusho: Kikokotoo cha biashara kimetolewa kwa madhumuni ya kielelezo pekee. Matokeo yanayowasilishwa na kikokotoo hiki ni kwa madhumuni ya mafunzo na ukadiriaji na hupaswi kuyategemea kuwa kamili na katika kufanya maamuzi ya uwekezaji. Matokeo ya wakati halisi yanaweza kubainishwa tu wakati wa utekelezaji wa agizo.

Jinsi ya kutumia pip calculator ya biashara ya Exness

Hatua ya kwanza

Chagua aina ya akaunti yako ya Exness na ubainishe leverage na sarafu ya akaunti yako.

Hatua ya pili

Chagua instrument yako ya biashara ambayo ungependa kwenye orodha inayopatikana.

Hatua ya tatu

Bainisha ukubwa wa lot wa trade yako na uendelee kukokotoa kwa kubofya kitufe cha 'Kokotoa'.

Maswali yanayoulizwa sana

Zana muhimu na rahisi kutumia, kikokotoo cha biashara ya Exness hukusaidia kukokotoa misingi ya trading position yako, ambayo ni pamoja na margin, gharama ya spread, ada, swap short, swap long na pip value. Kikokotoo hiki cha biashara chenye vipengele vingi ni muhimu sana unapotaka kukadiria thamani zilizo hapo juu kwa positions au orders kwa aina mbalimbali za instrument.

Kwa sasa kuna thamani 6 katika sarafu ya akaunti uliyochagua ambazo zitaonyeshwa na kikokotoo cha biashara:

  • Margin - Huu ni mtaji unaohitajika, au salio, unaohitajika ili kufungua position.
  • Gharama ya spread - Ni kiasi ambacho unalipa unapofungua position. Gharama ya spread inayokokotolewa hapa hutokana na wastani wa spread wa siku iliyotangulia ya biashara. Spread inapobadilika kwa kiwango kikubwa, kulingana na masharti ya soko, gharama ya mwisho ya spread inaweza tu kuamuliwa wakati position inafunguliwa. Pata maelezo zaidi kuhusu spreads za Exness katika sehemu ya akaunti za kutrade na kwenye kurasa za tovuti za masoko ambayo ungependa kutrade.³
  • Ada - Ada ni pesa zinazotozwa kwa kutrade kwenye akaunti za Raw Spread na Zero. Hutumika kwa kila lot inayofanyiwa trade na kwa kufungua na kufunga position. Thamani ya ada unayoona kwenye matokeo ya ukokotoaji ni ada ya jumla kwa pande zote mbili za trade (kufunguliwa na kufungwa), ambayo itatozwa wakati wa kufunguliwa kwa position. Ni muhimu kukumbuka kuwa kwenye jukwaa la biashara, spreads hujumuishwa kwenye ukokotoaji wa faida na hasara ya order, ilhali ada huonyeshwa kama gharama tofauti kwa kila order. Pata maelezo zaidi kuhusu ada za Exness katika sehemu ya akaunti za kutrade na kwenye kurasa za tovuti za masoko ambayo ungependa kutrade.
  • Swap short na long - Swap ni riba inayotozwa kwa positions za biashara ambazo zinaachwa zikiwa zimefunguliwa usiku kucha, na zinaweza kuwa long au short kulingana na trade. Swap short ni kiwango cha positions za Uuzaji ilhali swap long ni kwa positions za Ununuzi. Swap inapobadilika kwa kiwango kikubwa, kulingana na masharti ya soko, swap ya mwisho inaweza kubainishwa tu wakati ambapo positions zinachukuliwa kuwa zimeachwa zikiwa zimefunguliwa usiku kucha. Pata maelezo zaidi kuhusu swaps za Exness katika sehemu ya akaunti za kutrade na kwenye kurasa za tovuti za masoko ambayo ungependa kutrade.
  • Pip value - Hii huamua thamani ya pip moja, ambayo husaidia kukokotoa kiasi cha pesa ambacho trader atapata, au kupoteza, ikiwa bei ya trade itasonga kwa pip moja. Pip value hukokotolewa kwa sarafu ya bei kwa fomula, Lots x Contract size x Pip Size.

Matokeo yote huwasilishwa katika sarafu ya akaunti ya trader. Kulingana na instrument unayofanyia trade. Matokeo yanaweza kutafsiriwa kwa kutumia viwango vya ubadilishaji vya Exness vilivyo karibu na vya muda halisi.

Unapotumia kikokotoo cha biashara, leverage huwa imezimwa kwa baadhi ya instruments kwa kuwa zina leverage iliyowekwa awali. Katika hali kama hizi leverage haiwezi kubadilika na haiathiriwi na leverage kwenye akaunti yako ya kutrade

Kikokotoo cha biashara kimeundwa ili kutoa makadirio ya masharti ya biashara kwa order fulani, kikizingatia maelezo kama vile aina ya akaunti, sarafu, instrument ya biashara, kiwango katika lots na leverage. Huwa kinatumia data iliyo karibu na ya wakati halisi kutoa matokeo ya margin, ada, swap na pip value. Gharama ya spread ya kikokotoo hutegemea wastani wa siku iliyotangulia, na gharama za wakati halisi zinaweza tu kubainishwa wakati wa order execution. Kwa hivyo, ilhali kikokotoo ni zana muhimu ya kupanga na kukadiria, vipengee vilivyo hapo juu huathiri usahihi wake na traders wanapaswa kufahamu kuwa matokeo halisi ya biashara yanaweza kutofautiana.

Ndiyo, kikokotoo cha biashara kinaruhusu ukokotoaji wa matukio tofauti ya uwekezaji kwa kuzingatia vigezo kama vile aina ya akaunti, sarafu ya akaunti, instrument ya biashara, kiwango cha biashara katika lots na leverage. Hutoa matokeo kulingana na data iliyo karibu na wakati halisi, kwa ukokotoaji wa margin, ada, swap short, swap long na pip value. Hata hivyo, kikokotoo hiki hutumia thamani za wastani kwa gharama za spread, kwa hivyo gharama halisi zinaweza kutofautiana wakati order inatekelezwa kwenye soko.

Ili kukokotoa thamani ya pips katika biashara, tumia fomula:

Pip value = Lots x Contract size x Pip Size.

Ili kuamua thamani ya pip, kwanza, tambua pip size, ambayo kwa kawaida ni 0.0001 kwa jozi nyingi za sarafu, lakini kwa jozi na yen ya Japani, ni 0.01. Baada ya kuamua pip size, izidishe na ukubwa wa lot na contract size.

Pip value huonyesha thamani ya hatua ya pip moja katika trade na kusaidia traders kuelewa faida au hasara inayoweza kupatikana kutokana na mienendo ya bei. Huwa inakokotolewa kwa kutumia fomula: Lots x Contract Size x Pip Size, na huonyeshwa katika quote ya sarafu.

Long na short swaps hurejelea ada ambayo hutozwa kwa trading positions zinazowachwa zikiwa zimefunguliwa usiku kucha. Long swap ni kiwango cha ada kinachotozwa kwa positions za Ununuzi, ilhali short swap hutozwa kwa positions za Uuzaji. Kiwango halisi cha swap kinaweza kutofautiana kulingana na masharti ya soko na huamuliwa tu wakati ambapo position inachukuliwa kuwa iliwachwa ikiwa imefunguliwa usiku kucha.

Margin katika biashara ni kiasi cha mtaji kinachohitajika na trader ili kufungua trading position na hutumika kama pesa zinazowekwa kuonyesha nia njema zinazoshikiliwa na broker wakati wa trade.

Boresha jinsi unafanya biashara

Jionee mwenyewe kwa nini Exness ndiye broker anayefaa zaidi kwa traders zaidi ya 800,000 na washirika 64,000.