Habari za kampuni

Tunawaletea kiwango kinachofuata cha Exness

29 Januari 2024

Ili kusherehekea maadhimisho ya miaka 15, tunapeleka chapa yetu kwenye kiwango kinachofuata ili kuonyesha kile kilichotufanya kuwa broker mkuu zaidi wa rejareja duniani.

Kuunganisha na asili yetu

Katika Exness, tunashughulikia mambo kwa njia fulani. 

Kwa kila kitu tunachofanya, tunasawazisha teknolojia na maadili ili kutatua ukosefu wa ufanisi sokoni na kuwapa nguvu traders wetu. Tunafikia usawazisho huu kwa kutumia 'mawazo' na 'hisia' zetu Yote yanaunganishwa na maono moja: kufikiria upya jinsi soko la biashara linaweza kuwa.

“Ikiwa haipo, tunaivumbua. Ikiwa ipo, tunaiboresha.” – Petr Valov, Mwanzilishi na CEO, Exness

Tumevumbua, tukavuka mipaka, na kupinga hali ilivyo tangu siku ya kwanza. Sasa, miaka 15 baadaye, tumekuwa broker mkuu zaidi wa rejareja duniani. Tukiwa na zaidi ya traders 700,000 wanaoendeleza biashara, zaidi ya washirika elfu 64, na kiwango cha biashara cha kila mwezi cha hadi dola trilioni 4.8, tumefanikisha jambo la kipekee. Lakini huu ni mwanzo tu kwetu. Kuna mengi zaidi yajayo, na ni wakati wa kuboresha chapa yetu ili kuunganisha asili yetu na mustakabali wa biashara.

"Sisi ndio tunaongoza katika kila kategoria muhimu katika tasnia yetu, sasa ni wakati wa chapa yetu kuwa inayoongoza ulimwenguni pia." – Alfonso Cardalda, CMO, Exness

Kutana na EXO

Katika Exness, tunaamini kuwa kila kitu kimeunganishwa. 

Hali hii huwa halisi kupitia chanzo kimoja ambacho huunganisha chapa yetu pamoja.

exo

EXO ni mfumo mzima wenye maana kadhaa katika usawa

Ndani ya EXO kuna herufi za mwanzo zinazotambulika za Exness 'e' na 'x'. Inapozunguka, mduara unaowakilisha aikoni ya kichwa na moyo huonekana. Hii inawakilisha njia yetu ya kusawazisha teknolojia na maadili katika kila kitu tunachofanya.

Nembo ya kipekee na yenye muundo mzuri

Nembo mpya ya Exness imetokana na EXO. Herufi "e", "x" na "n" zimeundwa kwa kufuata usanifu wa kihisabati, na kusawazisha maumbo yaliyobinafsishwa ya "s" yaliyoundwa ili kusomeka kwa urahisi.

Upana thabiti na upau ulio katikati kabisa huleta usawa.

Rangi ya manjano inayoonekana vizuri zaidi

Rangi yetu ya kipekee ya manjano inafungamana sana na upekee wa Exness, na sasa hukuongoza kwa mambo muhimu zaidi. Rangi hii mpya inakamilishwa na seti mpya ya rangi iliyochaguliwa ili kuibua hali ya kujiamini.

Kiwango kinachofuata cha uzoefu wa chapa

Kwa kutokana na maumbo ya EXO, mifumo ya chapa yetu imeundwa ili kutoa kile unachohitaji —unapokihitaji. Kuanzia kwa kuzingatia kwa ufupi mawasiliano ya kiutendaji hadi kwa muonekano unaosisimua, tumeupa uzoefu wa watu kipaumbele.

"Chapa yetu mpya ina kusudi kwa kila kitu, na kila jambo lina kusudi." – Jennifer Van De Vooren, Mkuu wa Chapa, Exness

2024 itakuwa ya kipekee zaidi

Nyakati za kusisimua zinakuja. Jitayarishe kukutana na chapa yetu mpya katika kampeni zetu zijazo za uuzaji, taarifa za bidhaa na maonyesho ya siku zijazo. Tunapeleka chapa yetu kwenye kiwango kinachofuata, na utahusishwa kikamilifu.

“Kwa chapa hiyo mpya, mpango wetu ni kutumia uwezo wa maarifa yanayohusiana na data na simulizi bunifu ili kujenga miunganisho ya kweli na wateja wetu. Tunawaalika wateja kupata simulizi mpya ya kampuni, ambapo ushiriki wao utaunda mustakabali wa chapa yetu.” – Alfonso Cardalda, CMO

Je, ungependa kupata maelezo zaidi? Soma Maswali Yanayoulizwa Sana kuhusu kubadilisha chapa.


Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio ubashiri wa matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya trade kwa kuwajibika.