Maarifa

Je, uchumi wa Uchina uko hatarini?

Na Paul Reid

15 Mei 2024

is china facing a crisis

Kwa mara nyingine tena, vyombo vya habari vya Magharibi vinapendekeza kuwa uchumi wa Uchina unadorora, na hisia za soko la kimataifa tayari zinasababisha ushawishi kwa mali kadhaa zinazohusiana na Uchina. Lakini je, uchumi wa Uchina uko hatarini au ni propaganda tu za kuwaongoza wawekezaji wa soko la Asia kurudi kwenye masoko ya Magharibi?

Wacha tuangazie kwa undani zaidi madai kuwa uchumi wa Uchina unadorora na tuone ikiwa vichwa hasi vya habari 'vitakuwa leo... kesho vibadilike'.

Mgogoro wa mali isiyohamishika

Soko la manyumba linasemekana kuwa indicator kubwa uchumi wa nchi. Kulingana na ripoti ya gazeti la South China Morning Post, hisa za China Evergrande Group zilishuka kwa 79% baada ya kusitishwa kwa biashara kwa miezi 17. Kudorora kwa kampuni ya China Evergrande Group kunaashiria mgogoro unaoweza kutokea wa manyumba nchini Uchina, na hivyo kuonyesha masuala ya kimfumo kama vile nyumba kujengwa kupita kiasi, viwango vya udhibiti wa madeni, na ziada kubwa ya nyumba.

Mdororo huu wa kasi ulipunguza kwa kiasi kikubwa mtaji wake wa soko huku wawekezaji wakiitikia mchakato unaoendelea wa kampuni wa kudhibiti na kupunguza deni. Evergrande ni mhusika mkuu ambaye sekta nzima inategemea, kwa hivyo Evergrande inapokuwa ikipitia changamoto, unaweza kuwa na uhakika kwamba kutakuwa na athari kubwa na kuathiri imani na utulivu wa kifedha kote.

Soko la mali isiyohamishika la Uchina sio tu suala la kitaifa; ni la kimataifa. Mdororo Mkubwa wa Uchumi wa 2008/9 ulianza na kipindi cha bei za nyumba kupanda kutokana na ununuzi wa kubahatisha huko Marekani, jambo ambalo liliathiri hadi benki za ulimwengu. Ni vigumu kuelewa kuwa mdororo unaofuata wa ulimwengu unaweza kuanza nchini Uchina, lakini huo ni uvumi tu kufikia sasa.

Kumbuka kuwa kabla ya COVID, juhudi za ujenzi za Uchina zilikuwa zikikua kwa kiwango kikubwa. Kwa kuwa sasa mambo yametulia, huenda tunaona mabadiliko madogo ya mwenendo na sio mdororo mkubwa wa uchumi unaoathiri soko nzima.

Mgogoro wa ukosefu wa ajira

Kulingana na data ya mwisho iliyotolewa na Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Uchina, kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana katika maeneo ya mijini kilifikia kiwango kipya cha juu cha 21.3%. Viwango hivo viko juu sana sasa hadi maafisa waliacha kuviripoti, labda ili kuepuka kuibua wasiwasi kwa umma. Sheria kali, haswa katika sekta za kiteknolojia za kiwango cha juu zina wahitimu wachanga wanaopigania nafasi chache za kazi. Vijana waliosoma nchini Uchina wanapitia changamoto nyingi na hakuna dalili au matangazo kwamba hali inaweza kuwa bora.

Ukosefu mkubwa wa ajira pia ni kipimo kikubwa cha hali ya kiuchumi, lakini nchi ya Uchina sio nchi pekee inayokabiliwa na changamoto kama hizi, na ikiwa kila taifa lina suala la ajira, basi ushawishi wa mali ya Uchina unaweza kusawazishwa. Usawa wa aina hii unaweza kuwa maarufu zaidi katika jozi za sarafu, kwa hivyo usishangae ikiwa yuan itashindwa kuunda trend kwa sababu ya volatility tofauti.

Changamoto za kidemografia

Kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa, idadi ya watu nchini Uchina inapungua. Hili ni jambo ambalo halikutarajiwa katika ukuaji wa Uchina. Huku watu wengi wakiishi kwa muda mrefu zaidi, kuongezeka kwa idadi ya watu wazee huenda kukaathiri rasilimali za serikali. Pesa zaidi zitahitaji kuelekezwa kwenye ustawi na huduma ya afya, kupima uwezo wa fedha za umma.

Vilevile kwa ukosefu wa ajira, kupungua kwa idadi watoto wanaozaliwa na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaozeeka ni jambo ambalo nchi nyingi zinapitia. Mabadiliko haya ya kidemografia yanaweza kuchochea hisia hasi za soko na kuathiri bei, lakini changamoto zinazohusiana na kukua au kupungua kwa idadi ya watu ni nyingi na hazitakuwa kikwazo kikubwa kwa miaka kadhaa. Hata hivyo, ikiwa washiriki wa soko watasita sasa, watafunga positions zao, bila kujali kalenda ya matukio iliyotarajiwa.

Ushirikiano wa kiuchumi duniani

Uhusiano wa kiuchumi kati ya Uchina na washirika wake wakuu wa kibiashara, hasa Marekani na Umoja wa Ulaya, umekuwa na mvutano. Benki za Kichina zinaongeza uchunguzi kuhusu trade na Urusi kutokana na hofu ya vikwazo vipya vya Marekani, ambavyo vinaathiri kwa njia isiyo ya moja kwa moja trade kati ya Uchina na washirika wake wakuu.

Wataalamu wamejadili athari zinazoweza kutokea za Uchina kupunguza thamani ya yuan, ambayo inaweza kuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Marekani. Marekani inazingatia ushuru mpya kwa sekta ya Magari ya Kielektroniki na nishati ya jua kutoka China, ambayo inaweza kuwa na athari mbaya zaidi kuliko vita vya awali vya trade, hasa kama China inakabiliwa na vikwazo vya kutrade.

Kuibuka kwa China kama mdau wa uchumi duniani kumetatiza utawala wa awali wa Marekani na Umoja wa Ulaya na kusababisha mtandao tata wa trade, siasa za kijiografia na ushindani wa kiteknolojia. Licha ya mvutano huo, China iliipiku Marekani kama mshirika mkubwa wa kibiashara wa Umoja wa Ulaya mnamo 2020, ikiwa na trade yenye thamani ya $ bilioni 709, ikilinganishwa na thamani ya $ bilioni 671 za uagizaji na mauzo ya nje kutoka Marekani.

Mali unazopaswa kuangazia

Stocks kuu za kibinafsi kama vile Alibaba (BABA), Tencent (TME), na JD.com (JD) zinaweza kuathiriwa na hisia hasi. Makampuni haya huathiriwa na mabadiliko katika sera za kiuchumi za ndani na hisia za watumiaji.

Hong Kong 50 (HK50)

Kama mojawapo ya indices muhimu zinazowakilisha makampuni makuu ya Kichina yaliyoorodheshwa huko Hong Kong, HK50 inaweza kupata volatility kutokana na muundo wake mzito wa makampuni ya kifedha na mali isiyohamishika. Kudorora kwa soko la mali isiyohamishika la Uchina au changamoto za kifedha kunaweza kuathiri sana index hii.

USDCNY

Uchumi wa China unaotatizika kwa kawaida husababisha Yuan kuwa hafifu kadiri mtaji unavyotoka, na Benki ya Watu ya Uchina inaweza kurekebisha sera ili kudhibiti ukuaji wa uchumi. Jozi hii itakuwa tete haswa na kutoa fursa za kutrade kwenye mabadiliko ya muda mfupi ya bei na trends za muda mrefu.

AUDCNY

Kwa kuzingatia utegemezi wa kiuchumi wa Australia kwa Uchina, haswa kupitia mauzo ya bidhaa, Dola ya Australia mara nyingi huathiriwa na mabadiliko katika uchumi wa Uchina. Mdororo wa uchumi wa Uchina unaweza kupunguza mahitaji ya mauzo ya nje ya Australia, na kuathiri AUD kwa njia hasi.

Mafuta Ghafi

Kupungua kwa shughuli za kiuchumi za Uchina kunaweza kusababisha kupungua kwa mahitaji ya mafuta, na hivyo kuathiri bei ya mafuta duniani. Lakini fanya trade ya mafuta kwa tahadhari. Volatility ni jambo la kawaida kwa sasa, na kwa migogoro na shinikizo la hali ya hewa kupanda, kutakuwa na mambo mengi yasiyotarajiwa hivi karibuni. Nchi ya Uchina kwa kweli ni mwagizaji mkuu wa mafuta, lakini kutrade kwenye vichwa vipya vya habari vya ununuzi uliopungua wa Uchina sio jambo la busara. Ikiwa ungependa kutrade mafuta, zingatia mambo ya kimataifa.

Mtazamo wa traders

Fuatilia data ya PMI ya Uchina, ripoti za Pato la Taifa na habari za sera za serikali, kwa kuwa indicators hizi zinaweza kutoa dalili za mapema za mabadiliko ya kiuchumi. Zana kama vile moving averages, RSI, na MACD zinaweza kusaidia kutambua trends na points za mabadiliko ya mwenendo zinazoweza kutokea katika mali zilizotajwa.

Kwa kuzingatia uwezekano wa kuongezeka kwa volatility, kutumia stop losses na take profits kunaweza kusaidia kudhibiti hatari zinazohusiana na biashara katika nyakati hizi zisizo na uhakika. Kwa kuzingatia mali maalum, traders wanaweza kutafiti vyema hatari za kudorora kwa uchumi wa Uchina na kufanya trade ipasavyo.

Hitimisho

Kama kawaida, trader wanatarajiwa kuwa wanahisabati na wachunguzi wenye ujuzi na kila vyombo vya habari vya ulimwengu vikiwasilisha nadharia zake ambazo mara nyingi hukinzana, si rahisi sana. Ishara zote za awali za mdororo wa uchumi zipo, lakini sio kila mtu anafikiria kuwa ni halali.

Makala ya hivi majuzi kutoka Shirika la Habari la Xinhua yalionyesha hali ya matumaini zaidi kwa Uchina. Yaliripoti ukuaji thabiti wa Pato la Taifa wa 5.3% katika robo ya kwanza ya 2024, jambo ambalo inaonyesha uchumi thabiti na unaokua. Makala haya yanataja indicators zingine kadhaa chanya za kiuchumi, kama vile index thabiti ya wasimamizi wa ununuzi (PMI), trade ya kigeni inayostawi, na kuongezeka kwa uwekezaji wa mali halisi. Indicators hizi kwa pamoja zinapendekeza kuwa uchumi wa Uchina uko thabiti na labda unaonyesha dalili za kukua.

Lakini kumbuka, Upendeleo uko kila mahali, kwa hivyo kuona maoni chanya ya Uchina katika chapisho la Kichina sio jambo la kushangaza.

Inapendekezwa kuwa uchunguze kila mali kabla ya kuwekeza kutoka kwa vyanzo vingi kabla ya kuiongeza kwenye portfolio yako ya biashara. Zingatia kutumia Programu ya Exness Trade ili kupata taarifa mpya kuhusu bei za soko, kupata habari na ishara zilizojumuishwa, na ufikiaji wa soko mara moja kwa lengo la kunufaika kutokana na trends.


Huu sio ushauri wa uwekezaji. Utendaji wa awali sio ubashiri wa matokeo yajayo. Mtaji wako uko hatarini, tafadhali fanya trade kwa kuwajibika.


Mwandishi:

Paul Reid
Paul Reid

Paul Reid ni mwandishi wa habari za kifedha aliyejitolea kufichua miunganisho ya kimsingi iliyofichwa ambayo inaweza kuwapa traders faida. Akilenga zaidi soko la hisa, hisia za Paul za kutambua mabadiliko makubwa ya kampuni zimethibitishwa vyema kutokana na kufuata masoko ya kifedha kwa zaidi ya muongo mmoja.